Wakazi wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara Wabuni Mbinu Mpya ya Kukabiliana na Mafuriko

Wakazi wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara Wabuni Mbinu Mpya ya Kukabiliana na Mafuriko

Wakazi wa vijiji vitatu vya kata ya msitu wa tembo wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara kwa kushirikiana na wafadhili wameungana kukabili mafuriko kutokana na kingo ya mto Kukuletea kukatika na maji kusambaa katika makazi Yao.

Miongoni mwa wafadhili hao, kiwanda Cha uzalishaji sukari Cha TPC kinakadiriwa kutumia zaidi ya shilingi mil 92 katika kusaidia kujenga kingo ya mto huo ili maji yaeitawanyike na kusababisha mafuriko kwa wakazi hao.

Kwa zaidi ya wiki moja sasa, wananchi wa vijiji vya Londoto, Msitu wa Tembo na Kiruani wilayani Simanjiro mkoani Manyara walikumbwa na mafuruko baada ya mto huo kujaa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Wakizungumza mwandishi wa habari hizi baadhi ya wakazi wa eneo hilo Elisante Mwinuka, Marry Maiko na Eliwaha Mdeme wanasema wameamua kuungana kukabili mafuriko hayo kwa kuwa yaliathiri makazi Yao kwa kiwango kikubwa kwa kipindi Cha mwaka Jana(2020).

[Mkuu wa wilaya ya Simanjiro, Zepania Chaula akizindua zoezi la upandaji miti na nyasi katika vijiji vitati vilivyokubwa na mafuriko vya Londoto, Kiruani na Msitu wa tembo.]

Walisema mto huo ulikatika kingo kutokana na kuzidi kwa maji ya mvua yanayotitirika kutoka maeneo mengine ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa baadhi ya wakazi wenzao kufanya shughuli za kibinadamu pembezoni mwa mto huo.

"Kuna baadhi yetu bila hata kujali athari walivunja kingo za mto na kutengeneza mifereji ya kunyeshea mashamba yao kipindi Cha kiangazi Sasa mvua zilipoanza hawakuweza kurejesha kingo za mto zilivyokuwa matokeo yake tulipata mafuriko kwenye nyumba zetu" anasema Mwinuka

Akizindua kampeni ya upandaji miti zaidi ya 1,000 katika eneo hilo mkuu wa wilaya ya Simanjiro, Zephaniah Chaula alionya tabia ya kutofuata sheria ya kuacha mita 60 Kati ya mto na shughuli za kibinadamu ikiwemo ujenzi na kilimo.

[Wa kwanza kushoto ni karibu tawala wa wilaya ya Simanjiro, Zuwena Omari, akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya Simanjiro Zephania Chaula, akifuatiwa na Afisa tarafa ya Msitu wa Tembo, John Wambura.]

Mkuu huyo wa wilaya kwa kushirikiana na bodi ya maji bonde la Pangani (PBWB), kiwanda Cha TPC walishirikiana na wananchi na viongozi wa eneo hilo kupanda miti ili kuzuia kukatika kwa kingo za mto huo kwa Mara nyingine.

"Tuliunda kamati ya kupambana na mafuriko iliyohusisha wadau mbalimbali lakini kipekee niwashukuru kiwanda cha wukari cha TPC, bonde la maji mto pangani na mmoja wa wakazi wa eneo hili Mhandisi Emmanuel Manga wametoa sapoti kubwa sana" anasema

Akizungumzia kwa niaba ya menejimenti ya kiwanda Cha TPC meneja miradi wa kiwanda hicho Frank Mihayo anasema kiwanda hicho kitaendelea kushirikiana na wakazi wa eneo hilo kukabili mafuriko hayo kwani bado Kuna dalili za kukatika kwa kingo zilizowekwa.

"Tayari wakazi wa vijiji hivyo wameomba bado maji yanazunguka na kutaka kupita juu ya kingo tuliyoijenga hivyo ni ya kuboresha ili pia isije ukakatika na kuleta maafa ya mafuriko kama mwaka Jana..mvua zikipingua ndani ya siku tatu tutaleta mitambo ili kusaidia" anasema

Kwa upande wake msemaji kutoka PBWB mhandisi Arafa Majidi, anasema tayari wameweka alama ya mpaka Kati ya mto na shughuli za kibinadamu yakiwemo makazi ambapo alizitaka serikali za vijiji hivyo kuhakikisha miti inayopandwa hailiwi na wanyama lakini pia wanatunza vyanzo vya maji.

[Baadhi ya wakazi wa Kijiji Cha Londoto walishirikiana kuongeza kingo ya mto Kikuletwa.]

Awali, Afisa tarafa wa Msitu wa Tembo, John Wambura anasema bodi ya maji bonde la Pangani (PBWB), kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, wameokoa ekari za mazao mbalimbali, baada ya kudhibiti maji hayo.

Hata hivyo anasema eneo hilo lenye wakazi zaidi ya 7,000 ziliokolewa ekari 713 za mazao ya Mahindi,  Maharage, Nyanya,  Vitunguu, Biringanya, Bamia, Matikiti maji pamoja na Mpunga.