Barabara ya Kibwezi-Kitui Kuimarisha Uchumi Ukambani
Barabara ya kibwezi kuelekea kitui inatarajiwa kuleta mwamko mpya wa kiuchumi kwenye eneo la mashariki mwa Kenya kijumla.
Barabara ya kibwezi kuelekea kitui ni mojawapo wa barabara ambazo zinatarajiwa kuleta mwamko mpya wa kiuchumi kwenye eneo la mashariki mwa Kenya kijumla.
Mradi huo na ambao utagharimu serikari takribani shilingi billion 18.4 unatarajiwa kuinua hali ya maisha katika eneo la mashariki na haswa eneo la chini ya mashariki mwa kenya.
Barabara hiyo ina umbali wa kilomita 192. Mradi huo ulizinduliwa na raisi uhuru Kenyatta mwaka wa 2016 na unatarajiwa kukamilika mwenzi mei 2022.
Mradi huo utayaunganisha maeneo bunge 8 ukanda wa mashariki. Umeanzia kwenye makutano ya barabara ya Nairobi - Mombasa karibu na mji wa kibwezi na Kuelekea kaskazini kupitia Ikutha, Mutomo, Kitui, Kabati na Migwani.
Kenya imekuwa kwenye mstari wa mbele kufanikisha ajenda ya ujenzi wa barabara za hadhi za kimataifa. Kumbuka ili uchumi kunawiri lazima kuwe na usafiri mzuri na ambao utawezesha bidhaa kusafirishwa kutoka eneo moja hadi lingine bila matatizo.
Hii ndio sababu serikari ya Kenya imeipa sekta ya miundo msingi kipaombele kuhakikisha usafiri mwepesi nchini Kenya. Ujenzi wa miundo msingi ni nguzo muhimu ya Ruwaza ya 2030 ikiwemo ile ya usafiri kwa njia ya reli, barabara na huduma za majini.
Ukamilivu wa barabara hiyo utawezesha sekta ya Mali isiyohamishika(real estate) kukua kwa kiwango kikubwa. Usafiri ni msingi wa maendelea katika Kila sekta maana barabara hii itachangia ujenzi wa mahoteli makubwa na ya kifahari na pia nyumba za malazi kwenye maeneo husika.
Mradi huu unajitokeza kama muundo ambao utasukuma maendeleo ya kiuchumi na utangamano kwenye kaunti za mashariki na pia sehemu zingine nchini Kenya. Hii ni kwa sababu, barabara hiyo itatoa njia mbadala ya usafiri wa bandari ya mombasa hadi maeneo ya mashariki ya chini na juu na kupunguza msongamano katika barabara kuu ya Nairobi_mombasa. Barabara hiyo inaunganisha ile ya Mombasa-Addis Ababa ambayo inaungana na barabara kuu ya Nairobi-Addis Ababa huko Isiolo. Ni njia fupi mbadala hadi Moyale na hatimaye Addis Ababa, Ethiopia.
If you have a real estate press release or any other information that you would like featured on African Real Estate Blog Post do reach out to us via email at [email protected]