Mvua Zasababisha Uharibifu wa Miundombinu Chimala, Mbeya

Mvua Zasababisha Uharibifu wa Miundombinu Chimala, Mbeya

Kutokana na mvua zinazo endelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini zaleta kelo kwa wakazi wa maeneo  mbalimbali ikiwemo Chimala.

Mvua ina umhimu sana katika maisha ya mwanadamu ambayo hutumika kumwagilizia mazao ya wakulima wanao jishughulisha katika shughuli za kilimo kwa namna ya  kiasilia na kadhalika  mambo mengine.

Lakini japo tunasifia uwepo wa mvua na umhimu wake katika maisha  ya binadamu lakini hilo limekuwa ni kelo kwa wakazi wa Chimala walioko wilayani Mbarali mkoani Mbeya ambao ni wananchi wanao tegemea kilimo kwa asilimia 85% Kama vile kilimo cha zao la  mpunga na mazao mengine kwa kwa kiasi kidogo sana, zao hilo ndio linalo beba asilimia kubwa kwenye ukusanyaji  wa mapato wilayani Mbarali na kuongeza pato la taifa.

Mvua zinazo endelea kunyesha hivi sasa zimeweza kuharibu miundo mbinu mbalimbali Kama vile barabara, madaraja, nguzo za umeme, pamoja na uharibifu wa mazao yaliyo kwisha pandwa na wakazi wanaojishughulisha na kilimo.

Upande wa barabara wananchi sasa wanashindwa kufika kwa wakati katika mashamba kutoka na kuharibiwa kwa barabara hizo, kwahiyo  imekuwa ni chamgamoto kutumia vyombo vya moto Kama vile magari, pikipiki kusafiria kwenda mashambani mwao ambayo sasa wananchi hao hupaswa kutembea kwa umbali mrefu kufika mashambani na kupelekea  kupungua kwa nguvu kazi kutoka na upotevu wa mda.

Nilibahatika kuongea na wakazi wa kijiji  cha "Muwale"(Chimala), akiwemo mama  mmoja aliyefahamika kwa jina la Mama Rajabu ambaye ni mmoja wa waathirika kwa kipindi hiki akasema" barabara zimeharibiwa pamoja  madaraja hivyo imekuwa ni changamoto kwenda shambani amedai kuwa mda mwingine husubiri maji yapungue kwenye mito ili waweze kuvuka vivuko( daraja) baada ya madaraja  kusombwa na maji na hupelekea mazao kuendelea kuharibiwa kwa kukosa  kufika shambani na kushindwa kufanya matunzo ya mazao kwa wakati mwafaka kwahiyo kutakuwa na changamoto kubwa ya kupata mazao bora"

Rai ya wakazi hawa ni kwamba kwasasa hawana namna ila wanaishauri serikali yao baada ya kipindi cha mvua kuisha wanaomba kufanya ukarabati wa miundo mbinu Kama barabara na madaraja kwa ubora wa hali ya juu ili kuondoa adha wanao ipata kwa kipindi hiki.