Mbona Hoteli ya Gelian Yasifiwa Sana Machakos
Gelian hoteli ni hoteli ya kiwango cha juu mjini Machakos kaunti ya Machakos. Kwa muda sasa imepokea sifa nyingi kutoka kwa wateja ambao wamepata nafasi ya kuwa pale.
Hoteli hiyo inamilikiwa na aliyekuwa wakati mmoja mkurugenzi mtendaji wa shirika la ndege Precision Air Alphonse Kioko.
Gelian hoteli ni mojawapo ya hoteli mkubwa mjini Machakos. Ni hoteli ya nyota nne. Gelian hoteli ipo hatua chache kutoka Kenyatta Stadium na pia dakika chache kutoka uwanja wa gofu.
Hoteli hii ina vyumba vya kufanyia mikutano. Hii ni sehemu tulivu kwa wafanya biashara na ambao wanataka kufanya mikutano ya biashara. Kuna vyakula vya hadhi ya juu na kwa bei nafuu ambayo inajali mfuko wa mteja.
Hoteli ya Gelian inapeana huduma kadhaa kwa wateja wake kama vile; kidimbwi cha kuogelea kwa wageni wote na pia washiriki wa hoteli hiyo, kuna huduma za kusafisha nguo (laundry services), huduma za mtandoa kama Wi-Fi ya bure na sehemu ya kupaki gari.
Wafanyakazi wa hoteli hii ni watu ambao wanajua kufanya kazi yao kwa ufasaha na wanatoa huduma bila ubaguzi.
If you have a real estate press release or any other information that you would like featured on African Real Estate Blog Post do reach out to us via email at [email protected]