Mambo ya Kuzingatia ili Kujihadhari na Wadudu Hatari Majumbani

Mambo ya Kuzingatia ili Kujihadhari na Wadudu Hatari Majumbani
Picha: Mtandao

April na Mei ni miezi ambayo kunashuhudiwa hali ya mvua kubwa hususani katika jiji la Dar es Salaam.  Hali inayoambatana na joto kupungua pamoja na kutuama kwa maji katika sehemu mbalimbali.

Doreen Thadey mkazi wa Mikocheni anaelezea adha anayokumbana nayo katika kipindi hiki ambayo imewahi kuhatarisha maisha yake hapo nyuma.

"Kipindi hiki cha baridi ni kipindi ambacho wadudu hatari kama nyoka,ng'e na tandu wanakuwa wanaingia ndani ili kutafuta joto kutokana na hali hii ya kibaridi na wanaweza kukuuma."

Adha Doreen pia alieleza namna wadudu hao wanaweza ingia ndani ya nyumba. "Mfano mimi aliingia nyoka chumbani kwangu na alipita chini ya mlango kwani kuna uwazi kidogo na akapenya hadi ndani, ni hatari!"

Wadudu hawa wanaweza kudhibitiwa kwa kuziba kila upenyo ambao unaweza kinga wadudu hawa hatarishi kuweza kupenya na kuingia ndani kama Doreen anavyoshahuri.

"Nadhani kama ukishindwa kufit mlango vizuri ili kuziba nafasi basi weka tambara la deki mlangoni pindi uwapo ndani au utokapo. Pia kuna dawa za kufukuza wadudu hawa kama unaweza ni bora ukanunua." alisema Doreen Thadey.