Hoteli ya Kifahari A&L, Uzao wa Mapenzi
Hoteli ya kifahari, A&L inamilikiwa na Gavana wa Machakos na mpenziwe. Mwaka jana hoteli ya A&L ilikumbwa na upepo wa masaibu ya kubadilishwa jina baada ya wapenzi hao wawili kutalakiana.
Kaunti ya Machakos ni mojawapo wa kaunti ambazo zinakuwa kwa kasi sana. Kutokana na hali ya ukuaji wake, waekezaji wameanza kuekeza kwenye kaunti hiyo na haswa kwenye biashara za hoteli.
Gavana wa kaunti hiyo hajaachwa nyuma kwenye uwekezaji wa hoteli. Kwa sasa ni mmiliki wa hoteli ya kifahari ya A&L. Hoteli hiyo ni uzao wa mapenzi yake na aliyekuwa mkewe Lilian Ng'ang'a. Kwa sasa hoteli hiyo ni miongoni mwa hoteli bora katika kaunti ya Machakos na nchini Kenya kijumla. Hoteli hiyo ni kivutio kwa kila mmoja anayetamani kuzuru mji wa machakos. Jina la hoteli hiyo imetokana na jina ya wapenzi hao wawili wa zamani, A- Alfred na L- Lilian.
[Picha kwa Hisani]
Hoteli ya A&L iko kwenye barabara ya Machakos - Kitui, kilomita sita kutoka mji wa Machakos. Ni hoteli ya 5 -stars ambayo bali na vyumba vya kupata chakula ina vyumba vya malazi, kisima cha kuongelea, klabu na gadeni ya kupumzika baada ya kupata chakula chako na pia kupunga upepo. Kuna sehemu ya kupaki gari pia.
[Picha kwa Hisani]
Hoteli A&L ilifunguliwa mnamo tarehe 24 Julai mwaka wa 2020 na Gavana Alfred Mutua na aliyekuwa mkewe Lilian Ng'ang'a. Ikumbukwe wakati inafunguliwa ulimwengu wa biashara ulikuwa umeathirika pakubwa kutoka na janga la C0vid-19 lakini licha ya masaibu hayo, hoteli hiyo ilinawiri sana na kwa kasi ya juu.
Mwaka jana pia, hoteli ya A&L ilikumbwa na upepo wa masaibu ya kubadilishwa jina baada ya wapenzi hao wawili kutalakiana. Fununu zilienea kuwa Gavana Mutua angebadilisha jina la hoteli hiyo lakini mambo hayakuenda kulingana na hizo fununu. Alfred alisema kuwa hoteli ya A&L haitabadilishwa jina. Akizungumzia hali hiyo alisema, "kulikuwa na wasiwasi kuhusu jina la hoteli ya A&L, lakini mbona nibadilishe jina sasa? Hii bado ni hoteli yetu, wakati wazazi wanawachana, huwa wanawanyima watoto wao kutumia majina yao kwenye cheti cha kuzaliwa?"
Gavana Alfred Mutua na Lilian Ng'ang'a [Picha kwa Hisani]
Hoteli ya A&L ni hoteli ambayo kila mtu anatamani kupata chakula, hii ni kwa sababu limejengwa kwa namna ya kipee. Watu wengi wanaifananisha na 'White House' jina lililopewa jumba la kifahari la Gavana Mutua. Kama unampango wa kutembelea kaunti ya Machakos basi hakikisha unafika kwenye hoteli ya A&L na bila shaka utatambua kwa nini wanasema Machakos" is the best place to be."
If you have a real estate press release or any other information that you would like featured on African Real Estate Blog Post do reach out to us via email at [email protected]