Vyumba vya Mwanasoka Victor Wanyama

Vyumba anazomiliki mwanasoka Victor Wanyama

Vyumba vya Mwanasoka Victor Wanyama
Picha ya Victor Wanyama.

Pesa ni tamu wakati unazitumia kwa njia nzuri na ambayo inakufanikishia hali yako ya maisha. Hebu tafakari hili, kila mwisho wa mwezi unatia kibindoni shilingi zaidi ya millioni 20. Unaweza fanya nini na hicho kima kikubwa hivyo cha fedha?

Victor Mugubi Wanyama ni mwanasoka kutoka nchini Kenya. Amewai kuzichezea timu za Celtic, Tottenham Hotspurs, southmptom na Sasa anatekeleza majukumu yake na timu ya Montreal impact ya kutoka US.

Amekuwa nahodha wa timu ya Harambee Star kabla ya kustaafu kwake. Victor Wanyama ni mwekezaji ambaye ameekeza pesa zake hapa nchini Kenya na mataifa mbalimbali ulimwenguni.

Wanyama ni kati ya wanasoka kutoka Afrika ambao wanamiliki vyumba vya bei ghali. Mwanasoka huyu anamiliki nyumba nchini uingereza na pia hapa nchini Kenya. 

Nyumba nchini uingereza

picha/kumbukumbu

Victor Wanyama ana nyumba ya gharama ya juu sana katika jiji la london nchini uingereza. Fununu zinasema kwamba nyumba hiyo ilimgharimu mwanasoka huyo zaidi ya shilingi millioni sitini(ksh 60) pesa za Kenya.

Kwenye chumba hicho kuna nyumba kadha vya malazi, klabu ama baa, chumba cha kulia( dining hall) na pia Kuna kisima cha kuogelea. 

Nyumba nchini Kenya

picha/kumbukumbu

Wanyama anamiliki nyumba mtaani kileleshwa hapa nchini Kenya. Ni chumba ambacho uvutia macho ya kila mtu kutokana na uzuri wake.

Chumba hicho kina vyumba vitano vya malazi, chumba cha kulia, Kuna geregi tatu za magari, chumba cha kusomea, kisima cha kuogelea na ofisi.

Victor Mugubi Wanyama ndiye mchezaji wa Kwanza kutoka Kenya ambaye amewai kufunga bao kwenye michuona ya Klabu Bingwa Ulaya mwaka wa 2012 mwezi Novemba.

If you have a real estate press release or any other information that you would like featured on African Real Estate Blog Post do reach out to us via email at [email protected]