Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini Waanzisha Kampeni ya Weka Fukwe Safi
Mazingira ni vitu vyote vinavyo mzunguka mwanadamu kama vile mimea, vyanzo vya maji na vinginevyo binadamu anapaswa kuyatunza mazingira yake yanayo mzunguka ili mazingira hayo yaweze kumtunza pia.ukikata miti misitu ovyo hupelekea ukame hivyo kujikuta binadamu anaingia katika janga ambalo huathiri maisha yake kwa namna moja au nyingine.
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Tumaini kilichopo Mwenge ( Dar es salaam ) ambao wanasoma mwaka wa Kwanza wameanzisha kampeni ya "WEKA FUKWE SAFI" kama jitihada za kufanya fukwe kuwa Safi na salama kwa jamii.
Kupitia kwa mwenyekiti wa kampeni hiyo ambaye anajulikana kwa jina la "Peter Mganga" ni mwanafunzi wa mwaka wa Kwanza katika chuo hicho amesea walianzisha kampeni hiyo kwa lengo la kufanya fukwe kuwa Safi pia kuondokana na magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu, vile vile kuleta hamasa kwa jamii kutambua kuna haja kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ikiwemo makutano ya watu wengi mfano fukweni na maeneo mengine.
Aliongeza pia kuwa kampeni hii imeanzishwa mwaka huu (2021) ikiwa ina mda wa miezi takribani mitatu mbaka sasa wameweza kusafisha fukwe tofauti tofauti jijinini Dar es salaam ikihusisha wanafunzi na wasio wanafunzi pia alisema bwana Peter Mganga,kwa kuwa wanafunzi ndio watu wenye hamasa kubwa katika jamii ili kuleta matokeo chanya kutokana na hilo mwitikio wa watu kuungana kusafisha mazingira mbaka sasa unaleta matumaini watu tofauti tofauti wamekuwa wakijitokeza kuunga kampeni hiyo kwa kufanya usafi katika maeneo mbalimbali tajwa.
Lakini changamoto kubwa hawana fedha kwa ajili ya kununulia vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi kama vile kingamikono(gloves),vikusanyio vya takataka yaani (dustbins), chepeo au spedi, majembe, na vifaa vinginevyo.kutokana na uhaba huo wamekuwa wakishindwa kufanya usafi kwa ufanisi wa hali ya juu.
Tarehe 5 mwezi 5 kila mwaka ni siku ya mazingira duniani wanafunzi hao wamedai kuwa wataungana na watu wengine duniani kote kuadhimisha siku hiyo,hivyo watauungana na wakazi tofauti jijini hapa kufanya usafi katika mazingira tofauti tofauti.
Japo kuwa wanapitia changamoto mbalimbali hawajakata tamaa kuendelea kuelimisha jamii jinsi ya kufanya mazingira kuwa safi mda wote kwa vitendo na siyo maneno ili kuondokana na adha ya milipuko mbalimbali ya magonjwa na pia kupitia kampeni hiyo wanaamini kuwa wakipewa sapoti wataenda kuidondosha Rwanda kama nchi namba moja inayoongoza kwa usafi wa kimazingira Afrika Mashariki na kati.
Pia wameomba wizara ya mazingira nchini kujaribu kuangalia kampeni mbalimbali zinazo anzishwa na kufanywa na watu au mashirika ya siyo kiserikali kuwaunga mkono kwa jitihada mbalimbali wanazo zionyesha na kuzifanya kwa vitendo ili kufanya jamii kuonyesha mwitikio mkubwa ili kuifanya Nchi yetu kuingia kwenye nchi safi kwenye swala la utunzaji wa mazingira kama ilivo nchi ya Rwanda.
"TUNZA MAZINGIRA YAKUTUNZE"