Uwanja wa Mashujaa wa Nyayo

Uwanja wa kitaifa na kimataifa wa nyayo

Uwanja wa Mashujaa wa Nyayo
Photo/Courtesy

Kila wakati jina la uwanja wa Nyayo likitajwa, linaleta kumbukumbu kwa wapenzi wa michezo ya soka na riadha nchini Kenya, Afrika na ulimwenguni kijumla.

Ni uwanja ambao unathamani sana hata kwa soka ya hapa Kenya.

Uwanja wa Nyayo unatumika kwa matumizi mbalimbali ikiwepo soka na sherehe za kitaifa na kimataifa. Ni uwanja wa nyumbani wa timu ya AFC Leopard ambayo inacheza ligi ya hapa nchini Kenya.

Uwanja wa Nyayo ulijegwa mwaka wa 1983. Upo jijini Nairobi nchini Kenya. Umejengwa katikati ya barabara ya Mombasa, barabara ya Langata na barabara ya Aerodome.

Uwanja huo uko mkabala na Nairobi Mega mall, zamani ikijulikana Kama Nakumatt Mega. Uwanja huo una nafasi ya kuchukua takribani mashambiki 40,000.

Uwanja wa Nyayo hutumika kwa shughuli za michezo ya riadha, kuogelea na sherehe za kitaifa na kimataifa. Ni uwanja ambao una rasilimali nyingi sana zikiwemo ukumbi wa mazoezi na kidibwi cha kuogelea chenye urefu wa mita 50( hamsini). 

Kukamilika kwa uwanja huo kuliipa Kenya kuwekwa kwenye nafasi ya kitengo cha kuwania kuandaa michezo minne ya Afrika All- Africa Games mnamo mwaka wa 1987.

Mwaka wa 2010 ulipata nafasi ya kuchezewa michezo ya African Championship katika riadha.

Uwanja wa Nyayo ni uwanja muhimu sana kwa wakenya. Ni uwanja ambao umewawezesha wachezaji wengi kujulikani kimataifa na kuilitia nchi ya Kenya sifa nyinyi.

Mwaka wa 2009 uwanja wa Nyayo ulibadilishwa jina na kuita Coca Cola National stadium baada ya Kampuni kupata kandarasi ya kubadilisha jina la uwanja huo.

Miezi mitatu baadaye Kampuni ya Coca Cola ilijiondoa kwenye mkataba huo baada ya serikari ya Kenya kutaka uwanja huo kuitwa Coca Cola Nyayo National stadium jambo ambalo Coca Cola walilipinga na kupelekea kujiondoa kwao.

Serikari iliuita uwanja huo Nyayo National stadium baada ya Coca Cola kujitoa kwenye mkataba.

Jambo hilo liliwakasirisha wakenya na kuisuta serikari sana, wakenya walitengemea kuwa Kampuni ya Coca Cola ingeubadilisha uwanja huo na kuupa kiwango cha kimataifa ukilinganisha na serikari ya Kenya.

If you have a real estate press release or any other information that you would like featured on African Real Estate Blog Post do reach out to us via email at [email protected]