Kiwanda Cha TPC Chafanya Uwekezaji Mkubwa Kilimanjaro - Tanzania
Makala fupi kuhusu uwekezaji katika kiwanda cha uzalishaji sukari cha TPC kilichopo kaskazini mwa nchi ya Tanzania, katika mkoa wa Kilimanjaro.
Tanzania ina hekta milioni 44 za ardhi ya kilimo, na 5% tu ndiyo inayolimwa. Wawekezaji, huchuja uwekezaji wa kigeni, na huwezesha kuanzisha kwa mradi.
Nchini Tanzania, Sekta ya Kilimo ni muhimili wa maendeleo ya uchumi. Sekta hii inachangia kiasi cha nusu ya pato la Taifa, robo tatu ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi na chanzo cha chakula pamoja na utoaji wa fursa za ajira zaidi ya 75% ya Watanzania.
Kilimo kina uhusiano na sekta zisizo kuwa za kilimo kupitia uhusiano wa usafishaji kwenda kwenye usindikaji wa mazao ya kilimo, matumizi na uuzaji nchi za nje;Inatoa malighafi kwa viwanda na soko kwa bidhaa zilizotengenezwa. Tanzania inazalisha takribani 97% ya mahitaji yake ya chakula. Uzalishaji wa mazao ya chakula unatofautiana mwaka hadi mwaka kutegemea kiasi cha mvua kilichopatikana.
Ni katika Kiwanda cha uzalishaji sukari cha TPC kilichopo kaskazini mwa Tanzania kwenye mkoa wa Kilimanjaro umbali wa takribani kilomita 50 kusini mwa Mlima Kilimanjaro hulima hekta 8,000 za mashamba zinazozalisha tani 945,000 za miwa kila mwaka.
TPC yenye uwekezaji wa mtaji wa zaidi ya Sh Bil 226 ambazo zimetumika katika kuongeza uwezo wa kilimo cha Miwa, kuchakata miwa hiyo na kuzalisha Sukari kwa tani Zaidi ya 100,000 kwa mwaka.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kiwandani hapo na kumnukuu, Afisa mtendaji mkuu, Robert Baisac, Inaeleza TPC ilianzishwa mwanzoni mwa mwaka 1930, kwa jina la A/S Tanganyika planting Company limited na A.P Moller mfanyabiashara wa Denmark na ilisajiliwa rasmi nchini kama TPC Ltd mwaka 1973.
Ilipofika March 2000, TPC Ltd ilikuwa imebinafsishwa kwa shirika la uwekezaji lwa Sukari likijulikana kwa Kiingereza Sukari Investment Limited (SIL) ambayo ilinunua Hisa asilimia 75 katika kampuni ambapo asilimia 25 iliyobaki ilishikiliwa na serikali ya Tanzania.
Kwa mwaka wa 2021 wamezalisha Tani 103,000 na kupita malengo ya msimu uliopita wa kuzalisha Tani 95,000 ambao ulipata changamoto ya mwaka jana kwani walikumbwa na mafuriko na hivyo kuathiri baadhi ya mashama ya miwa sanjari na kuwa na ugonjwa wa Yellow sugar cane.
Mchango wa TPC kwa uchumi kupitia kodi, kama vile kodi ya huduma (Service Levy), Kodi ya ongezeko la thamani (VAT), Payee na kodi ya maendeleo ya shule zilifikia jumla ya Sh Bil 68.4 mwaka 2017 ikilinganishwa na Sh Bil 1.6 zilizorekodiwa mwaka 2000.
Anasema mchango wa TPC Ltd kwa serikali kwa maana ya Gawio ilikuwa kati ya Sh Bil 13.429 mwaka 2017 na kwamba gawio kwa serikali tangu mwaka 2004 hadi 2019 ni Sh Bil 74 ambapo kwa mwaka 2021 viwanda vyote nchini vilitoa Gawio la Kiasi cha Sh Bil 15.5.
Taarifa zinaeleza kwamba kiwanda cha Kilombero pamoja na ukubwa wake na serikali kuwa na hisa ya asilimia 25 bado hawajatoa gawio kubwa kama la TPC kwani Gawio linalotolewa na TPC ni zaidi ya mara mbili ikilinganshwa na lile linalotolewa na kiwanda cha Kilombero mkoani Morogoro.
Mapema akitoa taarifa Afisa mtendaji Utawala wa TPC, Jaffary Ally anasema TPC ni kwanda cha Mfano ambapo wamekuwa na mafanikio makubwa kwa kuongeza uzalishaji kutoka Tani 36,000 mwaka 2000 wakati wanabinafsisha hadi Tani 110,000 kinachozalishwa sasa.
Anasema mafanikio yanayopatikana yanatokana na kiwanda kuwekeza mtaji wa zaidi ya Sh Bil 226 ambazo zimetumika katika kuongeza uwezo wa kiwanda katika kuchakata miwa, uwezo wa mashamba katika kutoa miwa zaidi ambapo sasa utoaji wa miwa umefikia takribani Tani 140 kwa Hekta moja.
Ally anasema kiwango hicho ni bora miongoni mwa nchi zote zinazozalisha miwa duniani huku pia kiwango hicho ni moja kati ya viwango bora vitatu vya uzalishaji wa miwa duniani kila mwaka wanaangalia namna bora ya kukabiliana na ushindani wa uzalishaji wa sukari duniani.
Hata hivyo, Ally anasema jududi zinazoonekana sasa katika kiwanda cha TPC zinazotoakana na mazingira wezeshi yaliyoandaliwa na iliyokuwa serikali ya awamu ya tano chini ya aliyekuwa Rais, Hayati Dk Magufuli.
Anasema serikali ilitumia vyombo vyake mbalimbali katika kuhakikisha viwanda vya ndani vinalidwa kikiwamo cha TPC huku Hayati Magufuli akisiitiza suala la taasisi na kampuni hizo kutoa gawio kwa serikali kama njia kuu ya kuchangia uchumi wa Taifa.
Mnamo mwaka 2019, wakati wa Uhai wake, Hayati Dk Magufuli wakati akipokea gawio la Trilioni 1.05, alizipongeza taasisi, mashirika ya umma na kampuni 79 zilizotoa gawio na michango kwa Serikali. huku akitaka, mashirika ya umma na kampuni 187 ambazo hazikutoa gawio na michango kwa wakati huo, kutoa gawio na michango hiyo vinginevyo bodi zake zitavunjwa na uteuzi wa watendaji wakuu kutenguliwa.
Rais Magufuli amefafanua kuwa Serikali imewekeza mitaji ya kiasi cha shilingi Trilioni 59.6 katika taasisi, mashirika ya umma na kampuni 266 ikitarajiwa kuwa zitaendeshwa kwa tija badala ya kuwa tegemezi kwa Serikali ama kuendeshwa kwa hasara.
Akizungumzana taasisi hizo, alitaja takwimu kuhusu suala la Gawio ambapo alisema Mwaka 2015-16 yalikuwa 25 na yalikabidhi shilingi bilion 249, mwaka 2016-17 yalipanda hadi kufikia 38 na wakatoa gawio la shilingi bilioni 677 na kwa mwaka 2017-18 yalikuwa 40 na wakakabidhi shilingi bilioni 842 na kwa mwaka 2018-19 mashirika, makampuni na taasisi zimepanda hadi kufikia 79 wakitoa jumla ya shilingi Trilioni 1.05.
Serikali ilisisitiza kuwa utendaji kazi wa taasisi hizo ni moja kati ya vyanzo muhimu vinavyopaswa kuchangia katika maendeleo ya nchini ikiwemo miradi mikubwa inayotekelezwa nchini, na amerejea kauli yake kuwa kutokana na fursa zilizopo hapa nchini zikiwemo maji, ardhi, madini, gesi, mifugo na nguvu kazi, hakuna sababu ya watanzania kujiona masikini.
If you have a real estate press release or any other information that you would like featured on African Real Estate Blog Post do reach out to us via email at [email protected]