Matofali ya Kuchoma Yamekua Kimbilio kwa Watu wa Kipato cha Chini
Ujenzi wa nyumba ya matofali ya kuchoma umekuwa kimbilio kwa wakazi wa kipato Cha kawaida na cha chini na kuwafanya wamiliki nyumba ingawa matofali hayo yanatajwa Kama sio rafiki kwa mazingira.
Kadhalika utengenezaji wa matofali hayo na utumiaji wake umetajwa Kama chanzo kizuri Cha ajira kwani nyumba moja ya ukubwa wa wastani hujengwa kwa sio chini ya tofali 3,000 na kuendelea.
Wakizungumza na blog hii baadhi Kijiji Cha kiyungi Wadra Msangi, Elirehema Mvungi na Yusuph Shelukindo wanasema wameweza kumiliki nyumba kirahisi kutokana na upatikanaji wa matofali.
Mvungi anasema anafanya vibarua katika mashamba ya miwa Tpc hivyo kutokana na kipato chake Cha chini asingemudu kumiliki nyumba kwa ujenzi unaohitaji tofali za mchanga na sementi kwani ni gharama kubwa.
"Tofali hizi za udongo zilizochomwa zinauzwa Kati ya shilingi 150 hadi 300 lakini matofali yanayotengenezwa kwa mchanga na sementi Bei zake ni Kati ya shilingi 900 hadi 2,000 kwa tofali moja....Sasa nisingeweza kumiliki nyumba kabisa" anasema.
Kwa upande wao baadhi ya watengenezaji wa matofali hayo ya kuchoma, Kisa Mkwizu, Anna Phuza na Richard Lema wanashukuru uwepo wa biashara hiyo kwani imesaidia kupata kipato cha kuendeleza familia zao.
Awali akiongelea Aina hiyo ya matofali mtaalamu wa ujenzi injinia Ali Mrutu anasema ni matofali mazuri tu, iwapo yatachomwa kwa umakini na kuwa magumu kiasi cha kutoweza kupasuka kirahisi.
"Siwezi kusema matofali haya yana shida kubwa..isipokuwa yakijengewa yakiwa hajachomwa kwa umakini ujenzi wake hatakidhi viwango kwani huwa ni malaini, hupasuka na yanasababisha nyufa kubwa katika nyumba iliyojengwa" anasema.