Wananchi Wahofia Kudhuriwa na Ng'ombe

Wananchi Wahofia Kudhuriwa na Ng'ombe

Wananchi wa kituo cha Pugu jijini Dar Es Salaam waingiwa na hofu ya kudhuriwa na ng'ombe kimakosa baada ya ofisi za serikali ya taa kuhamishiwa ndani ya eneo la mnada wa ng'ombe jirani na kituo hiko.
Wananchi wa eneo hilo waliiomba serikali ihamishe ofisi hizo kwani inawapa hofu ya kudhuriwa na ng'ombe au kupoteza maisha.

Mkazi wa eneo hilo Bi. Aisha Waziri alisema kuwa, Ofisi za Serikali ya Mtaa kwa sasa zilipo ni ndani ya eneo la Mnada wa ng'ombe hivyo ikiwa mwananchi anashida inampasa apishane na wanyama hao ili kufikia ofisi hizo, "na mifugo hao kama tujuavyo kuna muda mwingine huwa wanakimbia hovyo na  wakikutana na mtu wanaweza kumdhuru, kwahio serikali inapasa itufikirie kwa hilo"aliongeza Bi. Aisha.

Mkazi mwingine wa eneo hilo Bwa. Joseph Masangula, alisema kuwa kama Serikali inajali usalama wa wananchi wake basi inapaswa kuhama eneo la Mnada na kutafuta eneo lingine kabla wananchi hawajapata madhara yoyote.

Kwa upande wa wafanyabiashara wa eneo hilo nao walikuwa upande wa wananchi kwani hata wao wanafanya biashara huku wakiwa hatarini lakini hawana jinsi kwa sababu ndio kazi inayowaingizia kipato.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kituo hicho cha Pugu, Bwa. Shukuru Mwinjuwa, alisema kuwa wapo katika harakati za ujenzi wa ofisi za serikali ya mtaa nje ya eneo la Mnada baada ya kupewa mifuko Hamsini ya Saruji kutoka kwenye mradi wa Yapi Merkez.

Chanzo cha Ofisi za Serikali ya Mtaa kuhamishwa ni kupisha ujenzi wa reli na barabara ambapo si Ofisi hizo tu bali na hata baadhi ya nyumba za Wanachi wa eneo hilo nazo zilibomolewa, huku Wanachi wakilipwa pesa na kwenda kujitafutia makazi mahali pengine.