Jinsi Thamani ya Ardhi Itakavyoonezeka Ujenzi wa Daraja la Kigongo-Busisi Utakapokamilika

Fursa zitakazotokana na ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi mkoani Mwanza ni pamoja ujenzi wa nyumba kwa ajili ya biashara, Bustani kwa ajili ya kufungia ndoa na sehemu ya kumbi za sherehe. Pia kuna fursa ya biashara Migahawa, Ofisi, na vituo vya kupiga picha, Nyumba za kupangisha kwa ajili ya maduka, Nyumba za kulala wageni (Guest Houses), na Bustani za kupigia picha.

Jinsi Thamani ya Ardhi Itakavyoonezeka Ujenzi wa Daraja la Kigongo-Busisi Utakapokamilika
Muonekano wa Daraja hilo likikamilika

Tanzania inatekeleza mradi wa ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi lenye urefu wa Kilometa 3.2 litakalounganisha wilaya za Misungwi na Sengerema mkoani Mwanza.

Daraja hilo linajengwa na kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) ya nchini China kwa gharama ya fedha za kitanzania Sh699 bilioni linategemewa kukamilika mwaka 2024.

Mwonekano wa daraja la Kigongo-Busisi litakapokuwa limekamilika mwaka 2024. Picha na Mgongo Kaitira

Pamoja na kurahisisha usafiri kati ya wilaya hizo mbili (Misungwi na Sengerema nchini Tanzania) kutoka kutumia wastani wa dakika 40 zinazotumika kuvuka eneo la Ziwa Victoria linalounganisha wilaya hizo daraja hilo linategemewa kudumu kwa miaka zaidi ya 100.

Fursa za Kiuchumi zinazotokana na daraja hilo

Miongoni mwa fursa zinazotokana na ujenzi wa daraja hilo ni pamoja na kununua maeneo ya kujenga nyumba kwa ajili ya biashara. Hii ni kwa sababu daraja hilo litakuwa na sehemu kwa ajili ya Wanandoa kufungia harusi hivyo kuwafanya wafanyabiashara wanaoishi karibu na daraja hilo kupata nafasi ya kufungua biashara zitakato ongeza kipato chao.

Biashara hizo ni pamoja na Migahawa, Ofisi za kupiga picha, Nyumba za kupangisha kwa ajili ya maduka, Nyumba za kulala wageni (Guest Houses), na Bustani kwa ajili ya kupigia picha.

Pia wakazi wenye maeneo kuzunguka lilipo daraja hilo watapata nafasi ya kuuza ardhi zao kwa bei kubwa kutokana na ongeeko la wateja wanaohitaji kujenga nyumba za biashara kuzunguka mradi huo.

Kuelekea ilipo Chato Mpya

Januari 13, 2021 Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Damas Ndumbalo aliitaja Chato mkoa wa Geita kuwa kitovu cha Utalii nchini Tanzania na maoni ya wachambuzi yanakisia kwamba miongoni mwa sababu zilizochangia waziri huyo kuitangaza wilaya hiyo kuwa kitovu cha utalii nchini Tanzania ni pamoja ujenzi wa daraja hilo ambalo litarahisisha usafiri kwenda katika wilaya hiyo yenye Mbuga ya Burigi Chato.

Pia wachambuzi wa masuala ya Kiuchumi wanashauri wawekezaji katika ardhi kujitokeza kwa wingi kununua ardhi katika wilaya zinazopitiwa na daraja hilo kabla rasilimali hiyo haijapata bei.

Miongoni mwao ni Rais wa Tanzania Dk John Magufuli ambaye alinukuliwa akiwashauri wakazi wanaoishi kuzunguka daraja hilo kuacha kuuza maeneo yao kiholela huku akiwataka kuwa na subira kwani kuna uwezekano yakapanda bei pindi daraja hilo litakapokamilika.