Waziri Aweso Ageuka Mbogo Mradi Hewa wa Bwawa la Zaidi ya Milioni 600

Waziri Aweso Ageuka Mbogo Mradi Hewa wa Bwawa la Zaidi ya Milioni 600
Picha/Kumbukumbu

SERIKALI imeagiza kukamatwa kwa watu watatu, akiwemo mdhibiti
Ubora wa wizara ya Maji kwa tuhuma za kuidhinisha malipo batili ya bwawa hewa la maji lenye thamani ya zaidi ya Sh Mil 630 wilayani Handeni mkoa wa Tanga.

Pamoja na watumishi hao, pia serikali imeagiza kukamatwa kwa mkandarasi ambaye alihusika katika ujenzi wa bwawa Hilo linaloonekana zaidi katika nyaraka na siyo uhalisia.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametoa agizo Hilo kufuatia kilio Cha wakazi wa kata ya Kwemkambala wilayani Handeni ,Diwani wa kata hiyo Kwamba upo ubadhirifu Unaosababisha wananchi kukosa maji safi na salama.

Katika agizo lake,Aweso ametaka kukamatwa kwa wataalamu hao akiwamo mtaalamu wa mabwawa kutoka wizara ya maji, mthibiti ubora na Mkandarasi wa mradi huo .

Anasema fedha hizo zilitolewa ili kukamilisha bwawa Hillo lililoanza tangu mwaka 2019/20 huku ukionyeshwa kukamilika kwenye taarifa ingawa alipofika eneo la tukio hakukuwa na mradi.

"Nimepokea taarifa kutoka kwa madiwani na wabunge kuhusiana na mradi huo lakini pia malalamiko ya wananchi kuwa hakuna bwawa nikasema nije na kweli bwawa hakuna.....sitaweza kukubali hili lazima nichukue hatua" anasema waziri huyo

Kwa upande wake diwani wa kata ya Kwedihamba Musa Abedi amesema wananchi wa eneo hilo walijitolea maeneo Yao kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo kutokana na adha walikuwa nayo tangu mwaka 2018 ambapo 2019 walikubali kutoa maeneo ili mradi huo ufanikiwe.

 "Inakatisha tamaa sana wananchi wametoa mashamba Yao tangu mwaka 2019 lakini mpaka sasa mwaka 2022 hakuna maji......tunaomba kwa aina hii ya utekelezaji wananchi Hawa walipwe fidia" anasema diwani huyo

"Ikiwa mkandarasi anaweza akalipwa Fedha zaidi ya milioni 300 na hajafanya chochote mpaka leo wananchi hawana maji nadhani ni vyema sasa wananchi wakalipwa fidia" anasema Musa

If you have a real estate press release or any other information that you would like featured on African Real Estate Blog Post do reach out to us via email at [email protected]