'Vishoka' Hawatambui Sheria za Ardhi Nchini Tanzania

Hujulikana kama 'vishoka' kwa majina mengine ila watu wengi wanapenda kuwaita madalali kutokana na uwezo wao wa kumuunganisha mteja na mwenye mali. Given Timoth Mwaitege ni moja ya vijana waliojiajiri kupitia shughuli hiyo japo ni mhitimu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam alipochukua shahada ya kwanza ya uandishi wa habari.

'Vishoka' Hawatambui Sheria za Ardhi Nchini Tanzania
Picha

Hujulikana kama 'vishoka' kwa majina mengine ila watu wengi wanapenda kuwaita madalali kutokana na uwezo wao wa kumuunganisha mteja na mwenye mali. Given Timoth Mwaitege ni moja ya vijana waliojiajiri kupitia shughuli hiyo japo ni mhitimu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam alipochukua shahada ya kwanza ya uandishi wa habari.

Kupitia uzoefu wake katika shughuli hizi za udalali Mwaitege ameweza kupata mtaji na kufungua biashara zake ndogo ndogo zinazomuwezesha kutokuwa tegemezi kwa wazazi.

Imekuwa ni desturi kwa watu wengi hasa maeneo ya mijini kutumia madalali kupata makazi ama vitu mbalimbali ikiwemo bidhaa za biashara na matumizi mengine ambayo inasababishwa na ongezeko la watu inayopelekea uhaba wa vitu hivyo. Madalali wamekuwa msaada mkubwa sana kwenye kutupatia vitu tutakavyo kwa urahisi ila je ushawahi jiuliza nafasi ya madalali katika sheria ya makazi nchini?

"Ni kweli madalali wengi hatuna ufahamu juu ya nafasi yetu katika sheria ya nchi na hii inatokana na asilimia kubwa yetu hawana Elimu" alisema Mwaitege, pale nilipomuuliza juu ya ufahamu wake juu ya nafasi ya madalali katika sheria ya makazi ya nchi akiongeza kuwa taasisi hii bado haijatambuliwa kama rasmi hivyo mtu yeyote ambae anaonekana ana ushawishi anaweza kuifanya tofauti na sekta nyinginezo ambazo wanachama wanakuwa wamejiandikisha.

Amina Kifura ni mama mwenye nyumba ambae mara nyingi hutumia madalali kumtafutia wapangaji wapya anasema "ni kweli madalali wamekuwa na msaada mkubwa hususani kwa sisi wenye nyumba wanarahisha kutupatia wapangaji na nadhani hiyo ndo nafasi yao kutuunganisha na wateja".

"Upangishaji wa nyumba au chumba unaendeshwa na Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 , ambapo sheria hiyo imetaja wahusika wawili tu katika upangishaji. Wahusika hao ni mpangaji na mpangishaji, sheria hii haijataja nafasi ya dalali, hivyo dalali anakuwepo kwa makubaliano kati ya mpangishaji au mpangishwaji". Anasema Jackline John (mwanafunzi wa sheria)

John anaongeza kuwa  dalali yupo kimakubaliano ya mmoja wapo kati ya wahusika wawili, makubaliano hayo yataendeshwa na sheria ya mikataba.Hivyo kwenye sheria hiyo dalali anatambulika kama wakala.Ambapo wakala ni mtu aliyeajiriwa kufanya kitu chochote kwa niaba ya mwingine, au kumuwakilisha mtu mwingine katika shughuli mbalimbali.Mtu ambaye anafanyiwa shughuli hizo au anayewakilishwa anaitwa "mhusika mkuu".